Siku ya leo tungependa kukuorodheshea faida kuu tano za Juice au chai inayotokana na Dried Rosella flowers katika mwili wa binadamu.
Kwanza kabisa fahamu ya kua Rosella ni moja ya mmea jamii ya Hibiscus ambayo hupatikana haswa katika Bara la Afrika na sanasana Afrika ya mangharibi lakini pia mmea huu hupatikana kwa uchache katika sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika ya Mashariki na kati.
Basi bila kupoteza muda ningependa nianze na faida za Juice au chai inayotokana na maua haya ya mmea wa Rosella:-
•Kupunguza msongo wa mawazo(hypertention):-Chai au juice inayotokana na Rosella inasaidia kwa kiwango fulani kupunguza msongo wa mawazo na hivo kuifanya akili ifanye kazi bila kupata shida .
•Ni kinga dhidi ya Maradhi au maambukizi mbali mbali;- Kwa namna moja Rosella inavirutubisho ambavo hivo husaidia mwili kuongeza kinga na kua imara dhidi ya maambukizi na magonjwa mbali mbali ya mwilini.
•Huimarisha mifupa iliyodhoofu(Osteoporosis):-Mifupa milaini au magonjwa ya mifupa hupelekea mtu kuvunjika au kupata tabu katika kutembea au kuchezesha viungo vyake kwa urahisi lakini Rosella juice huakikisha kwamba inaongeza uimara na kuyatibu maradhi ya mifupa kwa kua ina Vitamin D ndani yake.
•Hupunguza Maradhi ya moyo;- Ikiwemo mishtuko ya moyo na Moyo kuuma ,Rosella Juice inasaidia kuyapunguza na hata kuyatibu kabisa maradhi ya moyo kwa kua inapunguza msongo wa mawazo na hivo mtu huweza kuepuka maradhi hayo kiurahisi.
•Hutibu michubuko,vidonda au mikwaruzo mbali mbali ya kwenye ngozi mwilini;- kwa sababu ya uwepo wa Vitamin C katika juice ya Rosella ,ambayo kazi yake kuu ni kuijenga ngozi na kuifanyia marekebisho pale ilipoumia hivyo inasaidia kutibu vidonda vya mdomoni na mikwaruzo ya kwenye ngozi.