Sunday, August 19, 2018
Ukurasa wetu katika Instagram.👉s.e.t_industries
Unaweza kututembelea pia katika ukurasa wetu wa instagram kwa vitu vingi zaidi kila wakati kila mahali tunapatikana.
Thursday, August 2, 2018
Msimu wa nane nane.
Ewe mkazi wa Mbeya ni zamu yako sasa kuja kujionea bidhaa zetu hapo katika viwanja vya nane nane katika mabanda ya sido,kuanzia tarehe moja mwezi wa nane mpaka tarehe nane mwezi wa nane 2018.
Wednesday, May 30, 2018
Faida Kubwa za Asali ya S.E.T.
ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na mdalasini.
Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora.
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.
Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.
Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.
Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.
Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.
Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.
Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa kifungua kinywa.
Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganywa na mdalasini.
Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia. Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai iliyowekwa mdalasini na asali.
Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.
Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.
Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa ya kutibu saratani. Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi," anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.
Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9:00 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka," anashauri Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.
Asali inao uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.
Baadhi ya watu Marekani ya Kusini, wanasukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi ili kufanya harufu mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).
Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za asali na mdalasini, hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani. Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa. Lakini inayozungumzwa hapa ni asali mbichi ambayo inapatikana kwa wingi Tanzania, lakini tatizo kubwa ipo pia feki inayouzwa kama mbichi!
Kwa hisani ya AFYA.KWANZA
Tuesday, May 29, 2018
Asali ya nyuki wadogo sasa ipo sokoni.
Sasa S.E.T industry inawaletea asali ya nyuki wadogo yenye ubora na iliyo pakiwa katika mazingira safi na salama kuhakikisha inakufikia ikiwa salama popote ulipo kwa bei na ujazo unaoendana na mahitaji yako.karibuni sana mda wowote mahali popote.
Now S.E.T industry brings you Honey from stingless bees with high quality and which has been packed in a clean and safe environment for the users health safety,you can get it whenever you are in various packages with reasonable and affordable cost.you are all welcome any time anywhere.

Bidhaa halisi kutoka S.E.T industry
Afya yako yaweza kua safi kwa kuonja ladha ya bidhaa za asili kutoka S.E.T industries wasiliana na sisi ili kupata Asali ya asili, majani ya chai ya asili na maua ya Rossella mda wowote mahali popote +255 768 292 830
Your Health may be perfect with the taste of the natural products from S.E.T industries.contact us for Natural Honey, Natural Black tea and Rossella flowers any time any where +255 768 292 830
Your Health may be perfect with the taste of the natural products from S.E.T industries.contact us for Natural Honey, Natural Black tea and Rossella flowers any time any where +255 768 292 830
Saturday, April 21, 2018
Bidhaa mpya ya majani ya Chai ya Asili(Black tea)
Habari yako msomaji wa blog yetu, Katika siku ya leo tunapenda kuwaletea bidhaa yetu mpya ya asili ambayo ni Majani ya chai ya asili,(Black Tea) ambayo ni bidhaa yetu tunayo ichakata na kuipakia kwa usafi ili wewe mtumiaji wetu uweze kupata kitu cha asili, bora,halisi,salama na safi kwa matumizi yako na kea afya yako.
Bidhaa hii hupatikana hapa mjini Iringa kwa urahisi kabisa unaweza wasiliana na sisis kwa nambari za simu 0768292830 ili tukuetee bidhaa hiyo ya Tsh 1000/= na utaletewa mpaka ulipo.
Fuatalia kurasa ijayo ili kuzijua asili na faida za matumizi ya Majani ya chai ya asili yaani black tea kwa lugha ya kiingereza

Wednesday, March 28, 2018
Faida za kutumia Juice au chai inayotokana na Rosella
Hello msomaji wetu. Asante kwa kuchukua muda wako kuitazama blog yetu ya S.E.T industries.
Siku ya leo tungependa kukuorodheshea faida kuu tano za Juice au chai inayotokana na Dried Rosella flowers katika mwili wa binadamu.
Kwanza kabisa fahamu ya kua Rosella ni moja ya mmea jamii ya Hibiscus ambayo hupatikana haswa katika Bara la Afrika na sanasana Afrika ya mangharibi lakini pia mmea huu hupatikana kwa uchache katika sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika ya Mashariki na kati.
Basi bila kupoteza muda ningependa nianze na faida za Juice au chai inayotokana na maua haya ya mmea wa Rosella:-
•Kupunguza msongo wa mawazo(hypertention):-Chai au juice inayotokana na Rosella inasaidia kwa kiwango fulani kupunguza msongo wa mawazo na hivo kuifanya akili ifanye kazi bila kupata shida .
•Ni kinga dhidi ya Maradhi au maambukizi mbali mbali;- Kwa namna moja Rosella inavirutubisho ambavo hivo husaidia mwili kuongeza kinga na kua imara dhidi ya maambukizi na magonjwa mbali mbali ya mwilini.
•Huimarisha mifupa iliyodhoofu(Osteoporosis):-Mifupa milaini au magonjwa ya mifupa hupelekea mtu kuvunjika au kupata tabu katika kutembea au kuchezesha viungo vyake kwa urahisi lakini Rosella juice huakikisha kwamba inaongeza uimara na kuyatibu maradhi ya mifupa kwa kua ina Vitamin D ndani yake.
•Hupunguza Maradhi ya moyo;- Ikiwemo mishtuko ya moyo na Moyo kuuma ,Rosella Juice inasaidia kuyapunguza na hata kuyatibu kabisa maradhi ya moyo kwa kua inapunguza msongo wa mawazo na hivo mtu huweza kuepuka maradhi hayo kiurahisi.
•Hutibu michubuko,vidonda au mikwaruzo mbali mbali ya kwenye ngozi mwilini;- kwa sababu ya uwepo wa Vitamin C katika juice ya Rosella ,ambayo kazi yake kuu ni kuijenga ngozi na kuifanyia marekebisho pale ilipoumia hivyo inasaidia kutibu vidonda vya mdomoni na mikwaruzo ya kwenye ngozi.

Saturday, March 24, 2018
The S.E.T industry at the conference.
Katika siku ya jana tumehudhuria moja ya mikutano ya viwanda vidogo vya ujasiriamali hapa Iringa na tukio hili limetusaidia kujulikana na pia kupata mawazo na maoni na kuwajua watu mbalimbali na Fursa mbali mbali zilizopo hapa Iringa. pia katika mkutano huu tumeweza kuitambulisha bidhaa yetu ya pili ya asili ambayo ni Rosella Dried Flowers ikiwa ni bidha iliopokelewa vizuri na wateja wetu kutokana na Faida zake ambazo ni Kupunguza msongo wa mawazo,kutibu michubuko na vidonda vilivyopo mdomoni kwasababu ya uwepo wa Vitamin C katika maua hayo pale yanapotengenezewa Juice yake,pia Rosella husaidia kuimarisha mifupa,kutibu Ugonjwa wa moyo na ni kinga ya maradhi mengine .Bidhaa yetu ni halisi na Asili isio na kemikali yeyote Karibuni sana .
Kwa mawasiliano 0768292830.
Kwa mawasiliano 0768292830.
Friday, March 23, 2018
Dried Rosella Flowers
Habari zenu wasomaji,ni matumaini yangu wote ni wazima pia kwa sasa Kampuni ya S.E.T inawaletea bidhaa asili ya Dried Rosella Flowers yani Maarozella kwa bei ya Tsh 1000/= tu karibuni....Fatilia makala yetu ijayo kujua kazi ya Rosella na faida zake pia.
Tuesday, March 20, 2018
Membership Card za S.E.T industry
Habari yako ndugu msomaji, Pia tunashukuru kwaajili ya kutoa mda wako wa thamani kwa ajili yetu.
S.E.T INDUSTRIES sasa tunakuletea mfumo mpya wa Biashara ambapo sasa tunatoa Membership card kwa wateja na pia kwa mtu anaetaka kua wakala wa bidhaa zetu za Asili.Card hio itakuwezesha kupata gawio kila ifikapo mwisho wa mwezi kwa kutegemeana na kiwango cha bidhaa ulizo nunua na pia kulingana na Mauzo ya kampuni kwa mwezi husika Card hizo zinapatikana kwa bei ya Tsh1000/= lakini iwapo umeshanunua bidhaa moja wapo ya kampuni yetu na pia unaweza kuwasiliana na 0768292830 kwa urahisi zaidi ili kupata maelekezo zaidi.Pia Asali zetu hupatikana katika ujazo wa Robo lita,Nusu lita,Lita moja,Lita tano na Lita 20. Kwa bei nafuu kabisa. Karibuni sana.

Wednesday, March 7, 2018
Malengo Makuu ya kampuni ya S.E.T idustries
Changamoto katika jamii zimekua ni kero kubwa kwa wananchi ,lakini je ni nani wa kuzitatua changamoto hizi,je ni serikali,au ni sisi wenyewe wananchi.
S.E.T industries inamalengo ya kutatua changamoto hizi bila ya kutegemea serikali pekee bali ni kwa kutegemea wananchi wenyewe.
Kwa kupitia kuanzisha miradi mbali mbali kama vile kuogesha mbwa kwa kupita nyumba kwa nyumba,kufua nguo nyumba kwa nyumba,kusambaza vitafunywa na vyakula kwenye makampun binafsi na yasio binafsi na pia kupakia na kuchakata bidhaa asilia kama vile asali na zinginezo lakini pia kuanzisha mradi wa S.E.T community program ambao utaigusa jamii moja kwa moja ambazo kazi hizi ni vijana wenyewe tunaozifanya na hivo kutatua tatizo la ajira na changamoto tajwa hapo juu.
Lakini bila ya kuungwa mkono na jamii itakua ni vigumu kufikia malengi yetu ya kuongeza maendeleo na kutoa umasikini kwa jamii inayotuzunguka kwasababu vijana ndio nguvu kazi ya taifa letu.

- Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu hivo hatuna budi kuungana kwa pamoja tunaweza.
Sunday, March 4, 2018
Introducing S.E.T industry.
S.E.T industries deals with the packaging and processing of Natural products which include honey .
S.E.T industries ni kampuni inayojishughulisha na uchakatuaji na upakiaji wa bidhaa za asilia ikiwemo Asali
S.E.T industries ni kampuni inayojishughulisha na uchakatuaji na upakiaji wa bidhaa za asilia ikiwemo Asali
Subscribe to:
Posts (Atom)